Ushauri wa kiafya

Wakenya wameshauriwa  kuwa makini kuhusu vyakula hasa nyama  wanayokula ilivyopikwa ili kuzuia athari za kiafya.

Kwa mujibu wa utafiti ulofanywa na mtafiti Dkt Aabha Nagral wa Hospitali ya Apollo Navi Mumbai nchini India, mbinu nzuri za kupika yama ni kama vile kuchemsha ama kwa mvuke badala ya kukaanga kwa mafuta.

Kwa mujibu wa utafiti huo japo nyama ina madini mazuri ya Iron, Zinc na Vitamini madini hayo hupotea baada ya nyama hiyo kuhifadhiwa kwa muda mrefu ama kupakiwa. Kadhalika aina za nyama zinazojulikana  kwa kiingereza White Meat   kwa mfano kuku zimependekezwa zaidi.


Utafiti huo vilevile umebainisha kwamba wanaotumia nyama bila kufuata tahadhari za upishi na uhifadhi wako katika hatari ya magonjwa ya maini.
 

Akizungumza katika    mkutano wa Shirikisho la Madaktari Nchini lililoandaliwa jijini Mombasa Dkt Aaabha vilevile ameshauri dhidi ya chakula chochote kilichopitia viwandani.