Mwanahabari Kanze Dena ateuliwa kuwa Naibu Msemaji wa Ikulu

Mwanahabari Kanze Dena ateuliwa kuwa Naibu Msemaji wa Ikulu

Rais Uhuru Kenyatta amefanya uteuzi mpya wa maafisa wake wa mawasiliano katika Ikulu ambapo Mwanahabari, Kanze Dena ameteuliwa kuwa Naibu Msemaji wa Ikulu na Naibu Mkuu wa kitengo cha habari cha rais. Kanze atakuwa na majukumu ya kusimamia vitengo vya digitali, utafiti na mawasiliano.

Aidha atahusika katika kuimarisha uhusiano wa ofisi ya rais na wanahabari kwa lengo la kufanikisha agenda nne kuu za serikali. Aidha, aliyekuwa mwanahabari, Munira Mohammed ambaye amekuwa akihudumu katika ikulu kwa muda ameteuliwa kuwa  kiongozi wa  kitengo kipya cha makavazi na maktaba ya rais vilevile naibu kiongozi wa kitengo cha habari cha rais.