array(0) { } Radio Maisha | Maafisa wa polisi wametumwa shuleni humo kushika doria

Maafisa wa polisi wametumwa shuleni humo kushika doria

Maafisa wa polisi wametumwa shuleni humo kushika doria

Kufuatia kisa cha kubakwa kwa mwanafunzi katika shule ya wasichana ya Moi jijini Nairobi,waziri wa Elimu Amina Mohammed amevunja bodi ya shule hiyo,na kutangaza kujiuzulu kwa Mwalimu Mkuu wa Jael Mureithi

Waziri Amina aidha amesema maafisa wa polisi wametumwa shuleni humo kushika doria saa 24 kila siku hadi pale hali ya utulivu Itakaporejea.

Aidha amesema bodi mpya imeteuliwa kushikilia nyadhifa mbalimbali shuleni humo huku wahudumu wa maktaba,na wafanyakazi wengine wakipigwa msaSa upya.

Amina vilevile amewataka wazazi kufika shuleni humo saa nne unusu Alhamisi wiki hii ili kuwachagua maafisa wapya kuhudumu katika bodi ya shule.

Waziri huyo amewahakikishia wazazi kwamba usalama wa wanao umeimarishwa kikamilifu na wazazi wameshauriwa kuwarejesha wanao shuleni tarehe 10 Juni ili kuendelea na masomo yao.