Muthaura aapishwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya KRA

Muthaura aapishwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya KRA

Balozi Francis Muthaura ameanza majukumu yake rasmi akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru licha ya pingamizi zilizoibuliwa kufuatia umri wake. Muthaura ni miongoni mwa waliopishwa jana kuanza kuhudumu katika bodi hiyo katika Mahakama ya Juu jana.

Wengine ni wanachama walioteuliwa ambao ni Susan Mudhune, Charles Makori Omanga, Mukar Shah na Leonard Ithau. Mwanaharakati Okiya Omtata alikuwa ameelekea mahakamani na kufanikiwa kupata agizo la kuzua kuteuliwa kwa Muthaura kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Uajiri na Leba Byrum Ongaya.

Hata hivyo, jaji huyo baadaye aliondoa agizo hilo na kupisha kuapishwa kwa Muthaura