Mvua kubwa kushuhudiwa maeneo mbalimbali nchini

Mvua kubwa kushuhudiwa maeneo mbalimbali nchini

Kwa mara nyingine, Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga imetoa tahadhari kuhusu kipindi kingine cha mvua kubwa huku ikiwashauri wakazi wa maeneo ya Rift Valley, Kaskazini na Kati ya Nchi kujiandaa kwa mvua inayotarajiwa kunyesha kwenye maeneo hayo kuanzia Jumatatu hadi siku ya Jumatano. Idara hiyo imeonya kwamba huenda mvua hiyo ikasababisha mafuriko na kuwashauri walio nyanza za chini kuhamia maeneo yenye miinuko.


Miongoni mwa kaunti zinazotarajiwa kuathiriwa na mafuriko hayo ni Turkana, Marsabit, Samburu, Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Bungoma, Baringo, Nakuru, laikipia, Isiolo, Nyandarua, Kirinyaga, Meru, Tharaka Nithi, Embu, Kiambu, Nairobi, Murang’a na  Nyeri.


Wakazi wa kaunti hizo aidha wameonywa dhidi ya kutafuta hifadhi chini ya miti wakati wa mvua ama kutembea kwenye maeneo wazi ili kuepuka kupigwa na radi.