array(0) { } Radio Maisha | Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, Nairobi yafungwa kwa wiki moja

Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, Nairobi yafungwa kwa wiki moja

Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, Nairobi yafungwa kwa wiki moja

Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi jijini Nairobi wameondoka shuleni kwa likizo fupi Half Term kufuatia madai ya kubakwa kwa mwanafunzi mmoja shuleni humo usiku wa kuamkia jana. Hatua hii inafuatia agizo lililotolewa na Waziri wa Elimu Amina Mohammed, ambaye amesema shule itafungwa kwa kipindi cha wiki moja huku uchunguzi ukiendelea.

Aidha alisema atawaongoza maafisa wa usalama pamoja na wizara yake kuyakagua mazingira ya shule hiyo na kufanya ukarabati panapo haja ili kuhakikisha usalama umeimarishwa.

Haya yanajiri huku uchunguzi wa kisa hicho ukitarajiwa kuchukua mkondo mwingine baada ya madai kuibuka kwmaba huenda mwalimu Mkuu wa Shule hiyo alijaribu kumzuia mwanafunzi huyo kutopiga ripoti. Inadaiwa mwalimu Jael Murithi alimuahidi mwathiriwa kwmaba angegharamia masongo yake iwapo angesalia kimya.

Ikumbukwe wito umeendelea kutolewa kwa mwalimu huyo kuchukuliwa hatua kwani hiki sio kisa cha kwanza cha utovu wa usalama kuripotiwa shuleni humo.

Wanafunzi tisa walifariki dunia katika shule iyo hiyo Septemba mwaka uliopita kufuatia kisa cha moto, uliodaiwa kusababishwa na mwanafunzi mmoja wa shule hiyo.