Jumba laporomoka Nairobi

Idadi ya watu walioaga dunia kufuatia kis cha jumba kuporomoka mtaani Hurua imefikia wawili, baada ya mwili mmoja kupatikana. Watu wengine wanne waliookolewa baada ya jumba hilo la gorofa tano kuporomoka mtaani Huruma, jijini Nairobi wanaendelea kutibiwa.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu waliookolewa walikimbizwa hospitalini kwa matibabu, huku shughuli za kuwatafuta wengine wanaoofiwa kufukiwa ndani ya vifusi vya jumba hilo ikiendelea.

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kukabili majanga Pius Maasai amesema shughuli hiyo inaendeshwa na Maafisa wa polisi, maafisa wa Kaunti, Vijana wa Huduma za Vijana kwaTaifa NYS na wale wa Shirika la Msalaba Mwekundu.

Idadi kamili ya wale ambao wamefukiwa haijabainika.