array(0) { } Radio Maisha | Yemi Alade aahidi tamasha la kukata na shoka

Yemi Alade aahidi tamasha la kukata na shoka

Yemi Alade aahidi tamasha la kukata na shoka

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya tamasha za Choma na Ngoma zinazoandaliwa na Radio Maisha, mwanamziki maarufu wa Nigeria Yemi Alade ambaye tayari aliwasili nchini jana kwa tamasha hizo ameahidi tamasha za kukata na shoka hapo kesho katika Ukumbi wa Kimataifa wa  KICC, jijini Nairobi. Mwanamziki huyo hasa ameelezea furaha yake ya kushirikiana na Radio Maisha na kusema kwamba atahakikisha lengo lake la kuja humu nchini kuwatumbuiza mashabiki linatekelezwa kwa ukamilifu.


Mkuu wa Radio Maisha, Jom Japanni aidha amemshukuru Alade kwa kuitikia wito wa kuwatumbuiza mashabiki wa Radio Maisha na kuwaalika wote kwa sherehe hizo zitakazoanza kesho saa kumi na mbili jioni hadi che.

Aidha Mkurugenzi wa Marketing katika Shirika la Habari la Standard, Doreen Mbaya ameelezea mipango ya kuandaliwa kwa tamasha zaidi siku za usoni lengo likiwa kushirikiana na mashabiki wa Radio Maisha hata zaidi.

Mwanamziki wengine watakaotumbuiza katika tamasha ya Choma na Ngoma ni Sauti Soul the band, Kaligraph Jones, King Kaka, Willy Paul miongoni mwa wengine.