array(0) { } Radio Maisha | Wafula Chebukati amesema hatajiuzulu wadhifa wake, huku akiwalaumu makamishna watatu waliojiuzulu jana

Wafula Chebukati amesema hatajiuzulu wadhifa wake, huku akiwalaumu makamishna watatu waliojiuzulu jana

Wafula Chebukati amesema hatajiuzulu wadhifa wake, huku akiwalaumu makamishna watatu waliojiuzulu jana

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Wafula Chebukati amesema hatajiuzulu wadhifa wake, huku akiwalaumu makamishna watatu waliojiuzulu jana, akisema walishindwa kukubali mitazamo tofauti inayoibuliwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Chebukati amesema kila kitu ki shwari katika tume hiyo, licha ya kujiuzulu kwa Naibu wake Connie Nkatha Maina, Dkt. Paul Kurgat na Margaret Mwachanya. Anasema watatu hao hawakujiuzulu kwa hiari, bali sababu kuu ni uamuzi wake wa kumwajibisha Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo, Ezra Chiloba.

Kadhalika amesema walikuwa na fursa ya kuwasilisha malalamiko yao wakati wa mkutano wa dharura ulioandaliwa mjini Naivasha mnamo tarehe 13 mwezi huu, lakini hawakufanya hivyo. Vilevile amesema hakuna taratibu za kujaza nafasi nne zilizoachwa wazi.

Wakati uo huo, amesema chaguzi ndogo katika wadi za Kinondo na Ruguru zitaendelea na kwamba majina ya maafisa watakaosimamia chaguzi hizo yalichapishwa katika gazeti rasmi la serikali. Makamishna Abdi Guliye na Boya Molu ndio watakaozisimamia chaguzi hizo.