Sina Chuki na Jamii ya Abagusii, asema Rais Kenyatta

Sina Chuki na Jamii ya Abagusii, asema Rais Kenyatta


Sina Chuki na Jamii ya Abagusii, asema Rais Kenyatta
By Suleiman Yeri
Rais Uhuru Kenyatta amejitetea vikali dhidi ya kauli kuwa aliikosea heshima jamii ya Abagusii kwa kumshtumu Jaji Maraga akisema hana chuki dhidi ya jamii ya Abagusii licha ya kwamba anapinga uamuzi wa Jaji Mkuu, David Maraga wa jamii hiyo kwa kufutilia mbali ushindi wake.
Akihutubu mjini Nakuru katika kongamano la wajumbe kutoka Kaunti za Kisii na Nyamira, Uhuru amerejelewa kauli yake kwamba uamuzi wa Jaji Maraga ulimghadhabisha.
Aidha Rais Kenyatta ameongeza kuwa sababu ya kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu licha ya kuwa na imani kuwa alishinda ni kwa ajali ya amani. Vilevile ameapa kutoruhusu hali ya utulivu nchini kuathiriwa na harakati za wanasiasa.
Vilevile ameonekana kutetea hatua ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamanaji baada ya matokeo ya urais kutangazwa.
Kwa upanda wake Naibu wa Rais William Ruto amepongeza jamii ya Abagusii kwa kuwapigia kura nyingi na kurai kufanya hivyo tena wakati wa marudio ya kura za urais.