NASA kuanzisha machakato wa kuwashtaki waliotatiza uchaguzi

NASA kuanzisha machakato wa kuwashtaki waliotatiza uchaguzi

NASA kuanzisha machakato wa kuwashtaki waliotatiza uchaguzi
By  Careen Omae
Muungano wa NASA umeanza mchakato wa kuhakikisha kuwa hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wanaowatuhumu kutatiza uchaguzi wa Agosti 8. Akizungumza baada ya kikao cha wabunge wa NASA, mmoja wa vinara wa muungano huo, Moses Wetangula amesema jopo la mawakili likiongozwa na Seneta wa Siaya, James Orengo litakagua uamuzi wa Mahakama ya Juu na kuanzisha mashtaka ya binafsi wakitilia shaka ofisi ya Mkuu wa Mashtaka kwamba haitawachukulia hatua wanaohusika ama kuagiza uchunguzi.
Wakati uo huo, amesisitiza kwamba NASA itahakikisha marudio ya uchaguzi wa Oktoba tarehe 17 hayafanyiki, iwapo matakwa yao hayatashughulikiwa. Amesema wataendelea kushinikiza mabadiliko kufanywa hasa kuhusu mfumo wa uchaguzi nchini.
Jumanne wakati wa mkutano wake mataani Kibera, NASA vilevile ilisisitiza kuwa uchaguzi huo hautafanyika japo haujaeleza mbini zitakazotumiwa. Muungano huo umetangaza kuwa siku ya Jumapili, utaandaa mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa Jacaranda mtaani Dandora jijini Nairobi.
Ikumbukwe NASA imekuwa ikishinikiza maafisa hao akiwamo Afisa Mkuu Mtendaji Ezra Chiloba, Kaimshna Imaculate Kasaiti na Abdi Guliye kujiuzulu kwa kuwahusisha na dosari zilizokumba uchaguzi mkuu uliopita. Mapema leo, viongozi wa eneo la Kaskazini Mashariki wamemtetea vikali kamishna Guliye wakisema malalamiko ya NASA ni ya kisiasa tu.