"Rappers wa Kenya hawawezi kitu hata kheri rap ya Eric Omondi" asema Roma Mkatoliki

"Rappers wa Kenya hawawezi kitu hata kheri rap ya Eric Omondi" asema Roma Mkatoliki

"Rappers wa Kenya hawawezi kitu hata kheri rap ya Eric Omondi" asema Roma Mkatoliki
Wasanii wakali wa hip hop kutoka Tanzania wametua nchini kenya kusudi kutambulisha wimbo wao wa pamoja kwa jina ‘Hivi ama Vile’ ambao unatamba kwa sasa kwenye mitandao na media nyingi.

Wawili hao ambao wamedumu sana kwenye game la rap, wameelezea mambo mbalimbali waowaza kutekeleza ili kuimarisha muziki na pia kuleta heshima ya muzi wa hip hop kutokana na dhana kwamba ni muziki wa wahuni kama wavuta bhangi au maday ya kulevya.

“Hip hop sio mzuki wa wahuni ni tamaduni za jamii na lazima tuzingatie maadaili na kuelimisha jamii. Nashangaa watu wanasemaga eti hip hop inahusika na madawa ya kulevya mbona kuna watu mpaka wa soka wanatumia hiyo madawa sio tu bongo fleva hata pia bongo movie. Sema tu ni dhana ya watu sababu kati ya watu saba mmoja ni msanii wa hip hop na huyo pekee ndiye ataonekana hao wengine kwani sio walaguzi” akasema Stamina.

Roma ambaye anaskika kupitia wimbo wake ‘Zimbabwe’ ameeleza kuhusu album ya ngoma zao kwa pamoja ambapo tayari wimbo wao ‘Hivi ama Vile’ ndio wa kwanza kwenye album yao lakini pia kila mmoja atakua anafanya album kivyake.

Tuna album tayari tumeanza kuirekodi, ya kwanza ina nyimbo nane na collo yetu hii ndio ya kwanza hapo lakini pia tuna collabo na Ben Pol, Beka Flavour na wasanii wengine. Mimi nitafanya album ya kwangu na Stamina pia ya kwake, kwa ujumla ni album tatu” akasema Roma.

Roma amesema kuwa Stamina alimwambia kuwa rapper wa muziki Kenya hawezi kitu kheri rap ya Eric Omondi kitu ambacho huenda ni msimamo wao lakini wamekiri wazi kuwa Khalighraph Jones ametamba sana hadi anaskika Tanzania pamoja na King kaka, Nyashinski na Octopizzo.
Hata hivyo wasanii hao hawajaacha utani wao kwani Roma amemtania Stamina kwamba kitu anachokichukia kwake ni nywele zake mbaya huku Roma akimchana kwa kumwambia kuwa anachukia kitendo chake cha kuamka na kuvaa nguo zake kabla yeye hajaamka. Vilwe vile, Stamina amemsema Roma kuwa ni timu Vera Sidika na yeye (Stamina) ni timu Huddah Monroe walimbwende wa Kenya.

Na; Mitego Sasa.