Kutoka hotelini hadi kuwa msanii Kutoka hotelini hadi kuwa msanii

Kutoka hotelini hadi kuwa msanii Kutoka hotelini hadi kuwa msanii


Kutoka hotelini hadi kuwa msanii
Wasanii wengi wachanga wanapitia hali ngumu kabla ya kuweza kufikia malengo yao kama wasanii na kufanikiwa kuuza muziki wao kwenye soko bana la dunia.

Wengi walishakata tamaa lakini wapo wachache tu ambao wanazidi kujitahidi kuonyesha ulimwengu walichobarikiwa nacho na kufanya wawezalo kutanua mipaka ya kimuziki ili watimize ndoto zao. Muziki ni riziki kwa watu wengi japo kipaji wasanii wanahitaji kuonyesha uwezo wao kwa kupambana kufanya kazi nzuri ili kunasa kila sikio la mdau au shabiki.

JP Japolo msanii wa gospel amesimulia hadithi ya maisha yake kabla hajaingia studioni kurekodi muziki wake kwani aklkuwa akiangaika huko Rongai hajui wapi wala nani. Msanii huyo amesimulia changamoto zake kupitia Mitego Sasa Blog huku akionyesha kujituma na kujua malengo yake maishani.

“Safari yangu ya Muziki hijakuwa raisi ivyo changa moto imekuwa mingi sana kuingia studio ku record nilikuwa na tatizo mingi ju sikuwa na pesa ya kuingia studio  ila nilingangana sana nikatafta pesa kidogo Sp akanifanyia kazi moja 20/10 nakuambia nilizunguka na mziki huo nikifanyia maketing na sikuwa na juwa presenter yeyote bt nilikuwa na ulizia steshoni nikipeleka mziki yangu nilikuwa na toka rongai mguu mpaka taon kufika taon sikuwa najuwa niazie wapi so nilikuwa na ulizia watu wa taxi steshon flani iko wapi kisha wananieleza naenda uko nikifika na peana Mziki kwa gate na mawochi walikuwa wananiangalia na macho mbaya ju nilikuwa nime parara sana walikuwa wanashidwa uyu ni msanii mgani amechafuka ivi so walikuwa wakali kwangu lakini sikufa moyo nilijikaza sana” akaeleza JP.

Licha ya kuonekana mchakavu na walinzi wa stesheni za radio, Jp hajakata tamaa amepiga hatua na kurekodi muziki na sasa anajivunia uwezo wa Mungu kumfikisha hapo kwani alifanikiwa pia kupata producer akamfanyia video ya wimbo wake wa kwanza bure kwani hakua na uwezo wa kugharamia kazi hio.

“Ni Kuweka Mungu mbele kwa kilakitu nilikuwa na fanya baada ya miaka mbili nikahamia Saika kwenda kuishi na dadayangu ju Rongai maisha ilikuwa ngumu sana apo kwa hoteli flani nilikuwa nafaya kazi apo nikakutana na jama moja anaitwa kadema nilipo chapa na yeye story akaniambia kuna produce ana juwa nikamwambia anipele uko sikujuwa  ninani nilipo fika kwa studio nikapatana na Bizi B. Aliniskiza nakunifanyia kazi kwa bei nafu kisha akanifanyia video bure nakuambia iyo siku sikuwa ata na nguo ya maana ya Ku shoot video bt tulifanya ikawa safi nilitamba naiyo Mziki  nikaanza kujulikana na watu marafiki mbali mbili na nikaanza ku chapa mashow safari imekuwa iviyo mpaka sasa nisimame na yesu” yeye akamaliza hivyo Jp.

Kwa sasa msanii huyo ana video mpya ya wimbo wake ‘Nasimama Na Yesu’ ipo kwenye mtandao wa YouTube.

Na; Mitego Sasa