MWILI WA KASISI WAPATIKANA

Na Mike Nyagwoka

Polisi wanaendeleza uchunguzi kubaini mazingira yaliyosababisha vifo vya watu watatu ambao mili yao imepatikana katika sehemu mbalimbali nchini. Katika kisa cha kwanza, m wili unaokisiwa kuwa wa Mhubiri wa Kanisa la Kiadventisti katika Kaunti ya Nyamira aliyetoweka takriban mwezi mmoja uliopita umepatikana karibu na nyumba yake eneo la Nyansiongo. Kasisi Nicholas Kibagendi amekuwa akisakwa kwa mwezi mmoja sasa kabla ya vipande viwili vya mwili wake; kupatikana mita chache kutoka nyumbani kwake vikiwa vimeanza kuoza. Anthony Ogutu ni mkuu wa polisi eneo la Borabu.

Wakati wa kutoweka kwake mkewe alieleza kwamba alikuwa amepokea simu kutoka kwa watu wasiojulikana. Kwingineko  mili ya watu wawili vilevile imepatkana  katika mito miwili tofauti kwenye eneo bunge la Othaya.

Katika kisa cha kwanza, mwili wa mwanamume mwenye umri wa kadri ulipatikana katika bwawa la Chinga huku mwili wa mwanamke ukipatikana ukiwa unaelea katika mto Gikira. Polisi wanasema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa huenda mwanamume huyo alijiua kwa kujirusha katika bwawa hilo huku mwanamke huyo akishukiwa kusombwa na mafuriko hadi eneo hilo.