NASA YAELEKEA MAHAKAMANI KUPINGA ORODHA YA MAAFISA

NASA YAELEKEA MAHAKAMANI KUPINGA ORODHA YA MAAFISA

Na Carren Omae

Muungano wa NASA umeendeleza shtuma dhidi ya Tume ya uchaguzi IEBC, hata baada ya tume hiyo kutoa msimamo wake kuhusu rufa ailiyowasilisha mahakamani kupinga uamuzi wa awali wa mahakama kwamba matokeo yatakayotangazwa katika ameneo bunge kuwa ya mwisho wala sio ya muda, ambayo imepinga na NASA, muungano huo aidha umeibuka suala jingine ambalo huenda likazua mjadala zaidi.

NASA sasa umewasilisha kesi mahakamani dhidi ya IEBC, kwa madai kuwa iliwaajiri maafisa watakaosimamia uchaguzi katika kaunti bila kuwashirikisha washikadau wote. Kwenye ombi la dharura lililowasilishwa mahakamani Upinzani unadai hatua ya IEBC inakwenda kinyume na sheria.

NASA inadai haikufaa kwa IEBC kutovipa vyama vya kisiasa nafasi kuwasilisha hoja zao kuhusu uteuzi wa maafisa hao kwa mujibu wa sheria. Mbali na Hayo muungano huo unadai shughuli hiyo haikuwa wazi kwa umma.

NASA sasa inataka maafisa hao kutotekeleza majukumu