NASA yaisuta Jubilee

Na, Beatrice Maganga
Muungano wa NASA umeishtumu vikali serikali ya Jubilee kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha. Licha ya serikali kuanza kutekeleza mpango wake wa kupunguza bei ya unga wa mahindi, mgombea urais kupitia NASA,  Raila Odinga ameishtumu kwa madai ya kuwanufaisha wafanyabiashara wa mataifa mengine kupitia uagizaji mahindi na kuwatelekeza wa humu nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano wa NASA kwenye Kaunti ya Kisii, Raila aidha amesisitiza kwamba NASA itaanzisha kituo cha kujumlisha kura wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Raila amesema sharti matokeo ya urais yatangazwe katika maeneo bunge.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa urais Kalonzo Musyoka ameahidi kutekeleza kwa mabadiliko makuu nchini yakiwamo ya kielimu kiuchumi nakadhalika iwapo NASA itatwaa uongozi wa taifa wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti nane.