Nkaissery ahimiza kudumishwa kwa amani

Na Frederick Muitiriri

Waziri wa usalama wa nchi, Joseph Nkaissery amevilaumu vyombo vya habari kwa kukutokuwa na uzalendo. Katika kongamanao  la amani la siku tatu linaloandaliwa na mashirika tofauti, Waziri huyo amekosoa vyombo vya habari kwa kupeperusha masuala yanayoibuliwa na upinzani akisema baadhi ya masuala hayo yanahujumu usalama wa Nchi na ni ya uchochezi.
Kuhusu suala la uchaguzi mkuu mwezi Agosti,  Nksaserry amesema suala ibuka ni sehemu ambazo hakukuwa kunashuhudiwa ukosefu wa usalama yameanza kushuhudiwa sasa na kuwataka wakenya na viongzoi wote kuwa mstari wa mbele kudumisha amani.
Aidha amewataka viongozi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuna usalama nchini badala ya kuzua vvurugu kwenye mikutano yao. Kongamano hilo linaandaliwa kwenye hoteli moja hapa jijini Nairobi.