EACC YAANZA KUTATHMINI VYETI VYA WAGOMBEZI

EACC YAANZA KUTATHMINI VYETI VYA WAGOMBEZI

Na, Mike Nyagwoka/Beatrice Maganga
Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC imeanza kutathmini vyeti vya wagombezi wote watakaoshiriki uchaguzi mwaka huu.
Kwenye mkutano wa kutia saini mkataba na viongozi wa kidini kwa lengo la kufanikisha vita dhidi ya ufisadi, Mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukhala amesema tume hiyo itajizatiti kutekeleza jukumu lake kikamilifu licha ya changamoto za bajeti. Wabukhala ametoa mfano wa taifa la Hong Kong ambalo licha ya kuwa na watu milioni 7 pekee lina bajeti ya shilingi bilioni 30.
Wabukala ameelezea haja ya washikadau wote kuhusika katika mikakati ya kukabili ufisadi kwani athari za ufisadi ni msumeno unaokata kote.
Kiongozi wa Baraza la Waislamu SUPKEM, Adan Wachu kwa upande wake amelalamikia muda unaochukuliwa kabla ya kumhukmu mshukiwa wa ufisadi. Kadhalika, viongozi wa dini wamesema watakutana na Idara ya Mahakama ili kujadili suala hilo.