Mahakama yamzuia Joho kuhamisha pesa zako katika akaunti sita za CFC Stanibic

Mahakama yamzuia Joho kuhamisha pesa zako katika akaunti sita za CFC Stanibic

Na Carren Omae
Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho hana idhini ya kuzihamisha fedha zilizo katika akaunti zake 6 katika Benki ya CFC Stanbic, kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu. Akitoa uamuzi huo, Jaji Hedwing Ongudi amesema Joho ataruhusiwa tu kuzifikia fedha hizo baada ya uchunguzi dhidi yake kukamilishwa na Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA. Uamuzi huo unafuatia ombi lililowasilishwa mahakamani na KRA.

Mamlaka hiyo inamchunguza Joho kwa madai kwamba amekwepa kulipa kodi tangu mwaka 2014.
Wakili wa KRA, Sylvester Okello ameieleza mahakama kwamba rekodi zinaonesha kwamba Joho amelipia kodi tangu mwaka 2008-2013 pekee.

Ikumbukwe akaunti nyingine ya Joho katika Benk ya Diamond Trust inachunguzwa kwa madai sawa na hayo.
Vilevile anachunguzwa dhidi ya madai ya kugushi cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne KCSE.