Huduma Kenyatta kurejelewa

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA,

Huduma zote za afya katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta zinatarajiwa kurejelewa kikamilifu Jumatatu baada ya usimamizi wake kutia saini mkataba wa kurejea kazini na madaktrari wanaohudumu hospitali humo.


Ikumbukwe kuwa hospitali hiyo tayari imewarejesha kazini madaktari kumi na wawili ambao ilikuwa imewafuta kazi wakati walipokuwa wamegoma pamoja na kusitisha adhabu iliyopaswa kutolewa kwa madaktari wengine arubaini na wanane.


Aidha, usimamizi wa Kenyatta umesema kuwa hautowalipa madaktari mia mbili sitini na wanne mishahara ya miezi mitatu waliokuwa wamegoma huku ikiarifiwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa hospitali hiyo Lily Koros ameonywa kuwa atalazimika kugharamia fedha hizo iwapo ataidhinishwa malipo yao.