Ronaldo atangaza kustaafu

Na Andrew Shonko
Miaka sita iliyopita siku kama ya leo Februari 14, 2011 aliyekuwa mshambuliaji tajika wa taifa la Brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima almaarufu ‘Ronaldo’  alitangaza kustaafu kwake. Nyota huyo aliyefunga zaidi ya mabao 400 na kucheza zaidi ya mechi 600 ana mengi ya kukumbukwa.

Ronaldo alianza soka yake katika klabu ya Cruzeiro akiwa na umri wa miaka 16. Timu nyingine alizozichezea ni PSV Eindhoven, Barcelona,  AC Milan , Inter Milan, Real Madrid na akamalizia Corinthians. Ndoto ya wengi kumwona akicheza wingereza haikutimia baada ya jaribio la kujiunga na Manchester City kutibuka.  

Akiwa na umri wa miaka 16, Ronaldo alijumuishwa katika kikosi cha timu Brazil iliyoshinda kombe la dunia mwaka wa 1994 lililosakatwa nchini Amerika. Ronaldo alilichezea taifa lake jumla ya mechi 98 na kufunga mabao 62.
Ronaldo anajivunia mataji mengi ikiwemo mawili ya dunia , mawili ya Copa America na alitajwa mshindi mara tatu wa Ballon d’Or.