Wanyama ang’aa

Na Andrew Shonko
Mercy Wanyama, dadake mdogo nahodha wa timu ya Harambee Stars Victor Wanyama alionyesha mchezo mzuri baada ya kuiongoza klabu yake ya Equity Hawks kuwashinda wanabandari KPA 73-68 uwanjani  Nyayo Jumatatu usiku katika Ligi Kuu ya Kenya ya mpira wa kikapu na kuwapa taji lao la kwanza.  

Hili lilikua ni taji la kwanza kwa Equity Hawks, klabu ambayo ilianzishwa miaka mitatu ilyopita. Pambano hilo lililazimishwa kwenda muda wa nyongeza baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya 63-63 wakati wa muda wa kawaida. Wanyama aliyejiunga na klabu hiyo mwanzo wa msimu huu alipata vikapu 36 nao Evelyne Nora na Hilda Indasi wakichangia katika ushindi huo.