City yaishinikiza Chelsea

Na Andrew Shonko
 Manchester City walipunguza pengo baina yao na viongozi wa ligi ya EPL Chelsea hadi alama nane baada wa kushinda mechi yao hapo jana dhidi ya AFC Bournermouth .

Raheem Sterling aliweka City kifua mbele kunako dakika ya 29 naye Tyrone Mings akajifunga kunako dakika ya 69 na kufanya matokea kuwa 2-0. Hii inawaacha viongozi Chelsea wakiwa na shinikizo la kuendeleza uongozi wao baada ya kutoka sare ya 1-1 na Burnley hapo awali.