Gor, AFC kuchunguzwa

Na Andrew Shonko
NAIROBI, KENYA Kamati inayosimamia maadili ya FIFA, imeanzisha uchunguzi kwa klabu tatu za KPL kuhushu ukiukaji wa maadili wakati wa uhamisho wa wachezaji.


Gor Mahia, AFC  Leoprds na Sofapaka wameagizwa kufika mbele ya kamati hiyo ambayo inaongozwa na Kimberly Morris wiki ijayo. Wanakamati wa FIFA watakua wanafika humu nchini wiki hii ili kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo.

Mkurugenzi mkuu wa Gor Mahia Lodvick Aduda alidhibisha hilo lakini akasema ya kwamba hakuna lolote la kuogofya. Haya yanajiri huku kukiwa bado hakujaeleweka ni pesa ngapi ambazo klabu ilipokea baada ya kumuuza mchezaji Khalid Aucho ambaye sasa anachezea klabu ya Baroka ya Afrika kusini.
Bado haijulikani ni hatua gani zitachukuliwa dhidi yao iwapo klabu hizi zitapatikana na hatia ya kosa lolote.