Kombe la klabu bingwa Uropa larejea

Na Andrew Shonko
Kombe la klabu bingwa barani uropa litarejea usiku wa leo ambapo mechi mbili zimeratibiwa kusakatwa. Kombe hilo  linaingia awamu ya 16 ya mwondoano. Mabingwa mara tano wa kombe hilo FC Barcelona watakua ugenini dhidi ya Paris St Germaine ya Ufaransa.  Barcelona watakua bila huduma za Aleix Vidal aliyepata jeraha ilhali PSG watawakosa wachezaji Thiago Motta ambaye anatumikia marufuku yake  na Pastore aliye na jeraha. Mechi nyingine itasakatwa uwanjani Estádio do Sport Lisboa ambapo Benfica watamwalika Borussia Dortmond. Mechi zote zitang’oa nanga 10.45 usiku.