Bacary Sagna Matatani

Na Stephen Mukangai

Beki wa timu ya Manchester City Bacary Sagna amefunguliwa mashtaka na chama cha soka nchini England FA, kufuatia ujumbe wake wa uchochezi kwenye mtandao wa kijamii.

Baada ya mechi ya ligi ya premier dhidi ya Burnley  Sagna aliandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa wachezaji kumi dhidi ya 12 lakini tumefanikiwa kushinda.

SAGNA alitilia shaka umakini wa mwamuzi Lee Mason hasa baada ya kumwonesha Fernandinho kadi nyekundu.

Sheria za FA haziwaruhusu wachezaji kuzungumzia wamuzi hasa kwenye mitandao ya kijamii. Licha ya kuomba msamaha  Sagna amepewa hadi Ijumaa saa 3 Usiku kujibu mashitaka hayo.