KMPDU wapewa wiki mbili kukamilisha mazungumzo na wanachama

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Viongozi wa Muungano wa Madaktari, KMPDU wamepewa kipindi cha wiki mbili kukamilisha mazungumzoo na wanachama wake kuhusu kusitishwa kwa mgomo wao la sivyo wafungwe jela kwa mwezi moja.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji, Hellen Wasilwa amesema kuwa viongozi hao walikiuka sheria kwa kukosa kufika mahakamani jinsi walivyoagizwa na hivyo kuitoiheshimu mahakama.
Tayari serikali za kaunti zimeanza kuwaandikia barua madaktari wanaogoma wakitakiwa kueleza sababu za kuhisi kwamba hawafai kuchukuliwa hatua kwa kukataa kurejea kazini.
Madaktari wa Kaunti ya Nairobi, wana siku saba kufanya hivyo kabla ya hatua kuchukuliwa dhidi yao.

SIMILAR STORIES
Chebukati atwaa wadhifa wa Mwenyekiti IEBC
Chebukati atwaa wadhifa wa Mwenyekiti IEBC
Chebukati atwaa wadhifa wa Mwenyekiti IEBC
Uhuru kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
Uhuru kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
Uhuru kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
''Hatutakubali wizi wa kura'' Chasema Wiper
''Hatutakubali wizi wa kura'' Chasema Wiper
''Hatutakubali wizi wa kura'' Chasema Wiper

Comment Policy

comments powered by Disqus