Aliyekuwa Wakili wa Marehemu Mark Too atoweka

Aliyekuwa Wakili wa Marehemu Mark Too atoweka

Na Suleiman Yeri
Wakili aliyewasilisha kesi mahakamani kupinga mazishi ya mbunge maalumu wa zamani Mark Too na kutaka uchunguzi wa kina kufanywa ili kubaini kilichomuua mwendazake ametoweka.
Kwenye kikao na wanahabari mjini Eldoret,John Taalam ambaye ni nduguye wakili Lilan amesema mara ya mwisho kuwa na Lilan ni wakati alipokuwa naye mjini na kumwacha ndani ya gari akisema alikuwa akienda kutafuta pesa za kununulia mafuta ya gari ili kuelekea maeneo ya Ziwa katika kaunti ya Uasin Gishu.
Aidha familia ya Lilan imetoa wito kwa serikali kusaidia katika juhudi za kumtafuta wakili huyo ambaye alikuwa ameripoti awali kutishiwa kwa maisha yake baada ya mahakama kuu ya Eldoret kutoa agizo la kusimamisha mazishi ya Mark Too.
Afisa Mkuu wa Polisi Eldoret Magharibi, Samuel Mutunga amethibitisha kutoweka kwa wakili huyo na kusema alitoweka usiku wa Jumatatu, siku ya mazishi ya Too na hadi sasa simu yake imezimwa, huku akiisihi familia yake kutoa maelezo yatakayosaidia katika uchunguzi.
.............................