Rais Obama aahidi kumkabidhi mamlaka mrithi wake

Rais Obama aahidi kumkabidhi mamlaka mrithi wake

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Rais wa Marekani anayeondoka Barack Obama ameahidi kumkabidhi mamlaka mrithi wake Donald Trump kuambatana na matakwa ya katiba ya Marekani.
Akihutubu mjini Chicago wakati wa hotuba yake ya mwisho kwa Wamarekani akiwa Rais, Obama amesema kuwa atahakikisha taratibu zote zinazostahili zinafuatwa katika shughuli nzima ya kumkabidhi mamlaka Trumph huku akiwataka Wamarekani kujitokeza kutetea haki zao ikiwemo kuwachagua viongozi wenye matendo na wanaozingatia demokrasia.
Katika hotuba yake, Obama aidha amepigia upato utawala wake wa mihula miwili akisema kuwa alipiga hatua kubwa katika kuhakikisha raia wa Marekani wanapata huduma bora za afya kwa bei nafuu pamoja na kukabili suala tata la ugaidi.
Obama anatarajiwa kuondoka rasmi ofisini tarehe 20 mwezi huu baada ya kumkabidhi mamlaka Trump.