Jopo lililobuniwa kumchunguza jaji Tunoi lakosa kupendekeza hatua za kisheria dhidi yake

Jopo lililobuniwa kumchunguza jaji Tunoi lakosa kupendekeza hatua za kisheria dhidi yake

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Jopo lililobuniwa kumchunguza aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Juu Philip Tunoi limekosa kupendekeza hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi yake kwa kuhusishwa na sakata ya utoaji wa hongo ya shilingi milioni 200.
Jopo hilo chini ya uongozi wake Sharad Rao limemwambia Rais Uhuru Kenyatta katika ripoti yake kuwa halikuweza kutoa mapendekezo rasmi ya kutimuliwa kwa Tunoi au hatua nyinginezo dhidi yake.
Kwenye kesi hiyo, Mwanahabari Geoffrey Kiplagat alidai kuwa Tunoi alipokea hongo kutoka kwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero ili kutoa uamuzi uliomuegemea Kidero katika kesi iliyowasilishwa na Mbunge wa Kabete Ferdinand Waititu akipinga kuchaguliwa kwake katika wadhifa wa ugavana kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hiyo, inaarifwa Jopo hilo lililoteuliwa tarehe 23 mwezi Februari mwaka uliopita, limependekeza Uhuru aweke wazi ripoti yao.