Walinzi wa Joho na Kingi warudishwa

Na, Suleiman Yeri
Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi wamerejeshewa walinzi wao. Hata hivyo idadi ya walinzi hao imepunguzwa ikiliganishwa na awali.
Walinzi wa magavana hao wamerejeshwa baada ya malalamishi ya viongozi wa upinzani wakisema ni haki ya viongozi kikatiba kupewa walinza.
Wabunge wa Mombasa walikuwa wamempa Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Joseph Nkaissery makataa ya wiki moja kuhakikisha wawili hao wanarejeshewa walinzi wao huku wakisema kuondolewa  wao kulichochewa kisiasa.