Mahakama ya Mjini Eldoret,yakataa ombi la kusitisha mazishi ya Mark Too

Mahakama ya Mjini Eldoret,yakataa ombi la kusitisha mazishi ya Mark Too

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Mahakama ya Eldoret imetupilia mbali agizo lake la awali la kutaka kusitishwa kwa mazishi ya aliyekuwa mbunge maalum Mark Too.
Japo hakutoa sababu za kusitishwa kwa agizo la awali, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Eldoret, Nicodemus Moseti ameagiza waliotajwa kwenye rufaa iliyowasilishwa na wakili Simon Lilan kufika mahakamani tarehe 12 mwezi huu.
Mazishi hayo yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Uhuru, hafla itakayofanyika katika shamba la mwendazake la Mziwa, Kaunti ya Uasin-Gishu.