Mazishi ya Too kuendelea jinsi ilivyopangwa

Mazishi ya Too kuendelea jinsi ilivyopangwa

Na Frederick Muitiriri
 
Mwanamke aliyekuwa akitaka mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa Mark Too yasitishwe ameondoa kesi hiyo mahakamani. Hatua hii ni baada ya familia ya marehemu kukubali kumhusisha katika maandalizi ya mazishi hayo. Fatuma Ramadhan alidai kuwa Mark Too ni babake mwanawe wa miaka kumi na sita. Mahakama ilitarajiwa kuamua iwapo mazishi hayo ambayo yanatarajiwa kuwa nyumbani kwake Mjini Eldoret siku ya jumatatu yatasitishwa au la.
Fatuma alikuwa amewashtaki wajane ambao  walidai kuwa huenda mwanawe angeteseka sana iwapo hangeruhusiwa kumzika babake. Alidai kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa akimlipia mwanawe karo na kumpa mahitaji mengine ya nyumbani.
Tayari misa ya wafu imeanza katika kanisa la AIC milimani huku viongozi mbali mbali akiwemo aliyekuwa msajili wa mahakama Gladys Shollei akihudhuria.