Joho amsuta rais kwa mara nyingine
Na Beatrice Maganga
Gavana wa Mombasa Hassan Joho, amemsuta Rais Uhuru Kenyatta kwa kuizindua miradi kadha ya maendeleo anayodai haikuanzishwa na serikali ya Jubilee. Joho amesema miradi hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 2010 na iliyokuwa manispaa ya Mombasa wa si serikali ya Jubilee.
Gavana Joho amedai serikali inajaribu kuitumia miradi hiyo kujitafutia umaarufu na kusema mipango hiyo haitafaulu.
Miradi nyingine iliyozinduliwa ni kivuko cha Buxton na mradi wa kuimarisha miundo msingi wa Ziwa la Ng'ombe.