Mong'are azungumzia uteuzi wa IEBC

Na Caren Omae

Seneta wa Nyamira Kennedy Mong'are amesema ana imani na walioteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta katika nafasi ya Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi IEBC pamoja na Makamishna. Mong'are ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao, aidha amesema iwapo utaratibu mwafaka utafuatwa, walioteuliwa wana uwezo wa kuendesha shughuli hiyo inavyofaa.