Kamati kutathimini marekebisho kwenye sheria za uchaguzi na kuwasilisha ripoti Januari, 4

Kamati kutathimini marekebisho kwenye sheria za uchaguzi na kuwasilisha ripoti Januari, 4

Na Carren Omae
Kamati ya Sheria na Haki katika Seneti na ile ya Teknologia zina kipindi cha wiki moja pekee, kutathmini marekebisho katika sheria za uchaguzi na kuwasilisha ripoti. Katika agizo lake, Spika wa Bunge la Seneti Ekwee Ethuro amesema wakati wa vikao vyake, kamati hiyo itawahusisha washikadau wote, ikiwamo Tume ya Uchaguzi IEBC, Sekta ya Binafsi KEPSA, Mashirika ya Kijamii, viongozi wa dini na hata umma.
Wakichangia katika kikao maalum alasiri hii baadhi ya Maseneta hata hivyo, wameutaka Muungano wa CORD kusitisha maandamano dhidi ya kuidhinishwa kwa mapendekezo hayo, na bunge wiki jana, tarehe 4 Januari hadi ripoti hiyo itakapowasilishwa bungeni. Mutahi Kagwe ni Seneta wa Nyeri.
Hata hivyo Maseneta wengi wameunga mkono uamuzi huo wa Spika wakisema wanatarajia mwafaka utaafikiwa baada ya vikao vya kamati hiyo.
Awali baadhi ya Maseneta akiwamo Seneta wa Siaya James Orengo, Mwenzake wa Kakamega Bony Khalwale, Seneta Maalum Martha Wangare, miongoni mwa wengine, walipinga utaratibu wa vikao vya leo, suala lililopingwa na Spika katika uamuzi wake hivyo kuviwezesha kuendelea.