Washukiwa wa mauaji ya wakili Kimani wafikishwa kizimbani

Washukiwa wa mauaji ya wakili Kimani wafikishwa kizimbani

Na Sophia Chinyezi

Washukiwa watano wa mauaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi wamefikishwa mahakamani leo baada ya kesi dhidi yao kucheleweshwa kwa siku tatu.
Watano hao wakiwamo maafisa wanne wa polisi wa Utawala, Fredrick Leliman, Leonard Mwangi, Stephen Chebulet na Silvia Wanjiku, wamekana mashtaka dhidi yao. Mshukiwa wa tano Peter Kamau anaaminika kuendesha teksi ambayo watatu hao walitumia kabla ya kutekwa nyara na kuuliwa.
Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kwamba watatoa maelezo ya kutamausha kuhusu mauaji ya watatu hao, mbali na kutoa ushahidi utakaothibitisha kwamba washukiwa walihusika moja kwa moja na mauaji hayo. Watatu hao walitoweka Juni 23 baada ya kuhudhuria kikao cha kesi katika Mahakama ya Mavoko. Mili ilipatikana katika Mto Sabuk wiki moja baadaye.