Karua atangaza kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta

Karua atangaza kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta

Na Sophia Chinyezi

Kiongozi wa Chama cha Narc-Kenya, Martha Karua ametangaza kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika azma yake ya kuwania urais mwaka ujao. Wakati uo huo, amesisitiza nia yake ya kuwania kiti cha ugavana kwenye Kaunti ya Kirinyaga wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama chake cha Narc-Kenya.
Akizungumza katika Kanisa Katoliki la Kianyaga eneo la Gichugu mapema leo, Karua amesema amechukua uamuzi huo kwa kuwa ni chaguo la watu wa Kirinyaga. Ameongeza kuwa Rais Kenyatta amejitolea kupiga vita ufisadi na kuahidi kuunga mkono jitihada zake.