Jengo laporomoka Kisii huku manusura wakiendelea kutafutwa

Jengo laporomoka Kisii huku manusura wakiendelea kutafutwa

Na Beatrice Maganga

Watu wawili wameripotiwa kufariki dunia kufuatia kuporomoka kwa jengo moja mjini Kisii. Kulingana na Gavana wa kaunti hiyo James Ongwae, watu takriban thelathini wamejeruhiwa katika kisa hicho. Mmoja ameripotiwa kuwa na majeraha ya kichwa huku mwingine akijeruhiwa kiunoni.
 Kulingana na Ongwae manusura wanatibiwa katika hospitali mbalimbali za kaunti. Shughuli ya kuwatafuta manusura zaidi hata hivyo inaendelea.
Jengo hilo lililokuwa bado linajengwa aidha liliyaharibu majengo mengine mawili yaliokuwa karibu.