Brigedia Fatumah Ahmed, aapishwa mbele ya Rais Kenyatta kuwa mwanamke wa kwanza katika wadhifa wa Meja Jenerali katika jeshi.

Brigedia Fatumah Ahmed, aapishwa mbele ya Rais Kenyatta kuwa mwanamke wa kwanza katika wadhifa wa Meja Jenerali katika jeshi.

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla ya kuwapandisha vyeo wakuu wanne wa Idara ya Jeshi kuvisimamia vikosi mbalimbali vya idara hiyo, hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi.

Miongoni mwao ni Brigedia Fatumah Ahmed ambaye ataingia katika historia ya jeshi kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Meja Jenerali katika kikosi hicho. Rais Kenyatta amempongeza kwa uteuzi huo na kumsihi awe kielelezo katika idara hiyo na kwa wanawake wote.

Rais aidha amesema serikali yake itaendelea kuhakikisha kikosi hicho kinapata rasilmali zinazohitajika ili kuwahudumia wananchi kwa ukamilifu. Kulingana na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua, majenerali  hao walipendekezwa na Baraza la Idara ya Jeshi kuhudumu katika nyadhifa hizo.
Wengine walioapishwa ni Luteni Jenerali Robert Kariuki, Meja Jenerali, Francis Ogola na Luteni Jenerali W Raria Kopiaton.