array(0) { } Radio Maisha | Ruto na Kalonzo wazidi kuapa watafanyakazi pamoja

Ruto na Kalonzo wazidi kuapa watafanyakazi pamoja

Ruto na Kalonzo wazidi kuapa watafanyakazi pamoja

Naibu Rais William Ruto na Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka wamezidi kuelezea kujitolea kwao kufanya kazi pamoja licha ya tofauti zao za kisiasa.

Wakikutana katika hafla moja tangu hafla ya maombi ya kitaifa Mei 31 wawili hao wamesisitiza kuwa ushirikiano wao ni kwa minajili ya umoja wa taifa

Wakihutubu wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Gavana wa Kaunti Nairobi, Mike Sonko, Naibu Rais amemrai Kalonzo kuwapuuza wale wanaodai kuwa amejiunga na serikali kwa sababu ya kuchukua hatua hiyo ya kukubali kushirikiana na serikali.

Aidha Ruto amesisitiza kuwa wakati wa siasa umekamilika na kuwataka wanasiasa kukumbatia ushindani wa maendeleo na sera badala ya kuwagawanya wakenya kwa misingi kikabili.

Kwa upande Kalonzo licha kushikilia kuwa naunga kono ushirikiano hao amesisitiza kuwa upinzani ubgali imara na hautasita kuikosoa serikali pale inapoenda mrama akitolea mfano ongezeko la visa vya ufisadi amabvyo vimekithiri nchini.

Gavana wakati uo huo amewahakikishia wakazi wa kaunti hii kuwa atatekeleza hadi alizowapa wakazi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu na kuwa utawala wake utashirikiana na serikali kuu katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili.

Wito amabao umeungwa mkono na Ruto amabaye amefichua kuwa Nairobi itakuwa ya kwanza kunufaika na ajenda kuu utawala wa jubilee kwa kujengwa kwa makazi ya bei nafuu.