array(0) { } Radio Maisha | Maadhisho ya Hypertension
Maadhisho ya Hypertension

(Picha kwa hisani)

 

Kila mwaka tarehe 17 mwezi Mei hutengwa kuadhimisha Shinikizo la damu mwilini kwa Kiingereza High Blood Pressure au hypertension. Ugonjwa huo ni moja wapo ya magonjwa ambayo watu wengi wameyahusisha na uzee, uzani kupita kiasi na hata matajiri.

Watu bilioni 1.1 duniani wana tatizo la shinikizo la damu mwilini, kumaanisha miongoni mwa watu mia moja, ishirini na wawili wana tatizo hilo, vilevile miongoni mwa ishirini na wawili hao, ni wanne pekee ambao wamedhibiti ugonjwa huo.

Kulingana na utafiti wa kiafya, watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda wako katika hatari kubwa ya kuwa na ugonjwa huo kutokana na ulavi vyakula vya bei rahisi hasa vile ambavyo huuzwa kandoni pa barabara. Miongoni mwa vyakula hivyo ni viazi karai, bhajia, mutura na soseji zinazonunuliwa kwa shilingi ishirini tu.

Wakati wa maadhimisho kama haya mwaka jana Radio Maisha ilimhoji Dakta Kwaye Omondi ambaye alifafanua sababu  zinazochangia ugonjwa huo. Alieleza kuwa kukosa mazoezi, ulaji nyama kwa wingi, uvutaji sigara, mawazo mengi, umri na kama ugonjwa huo uko katika familia. Vilevile wanawake wajawizito huwa katika hatari kubwa.

Kaunti zilizorekodi visa vingi vipya vya hypertension ni Murang'a, Embu, Tharaka Nithi, Lamu na Makueni. Huku Kaunti za Turkana, Pokot Magharibi, Samburu, Mandera na Wajir zikirekodi idadi ya chini.

Muranga, Embu, Tharaka Nithi, Lamu and Makue
Read more at: https://www.standardmedia.co.ke/health/article/2001280789/100-000-die-annually-from-hypertension-complications

Aidha, watu wengi huchelewa kugundua kwamba wanaugua hypertension kwani ugonjwa huo hauna dalili na huambatana na magonjwa mengine. Vilevile ugonjwa huu unaweza kuthuru vyungo vingi mwilini kabla ya kugunduliwa.

Utafiti unaonesha kuwa mtu akiwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu, anaweza kuanza kutokwa na damu mwilini kwani hali hiyo inaweza kusababisha mpasuko wa mishipa ya damu. Vilevile mishipa ya kusafirisha damu hupanuka na kuwa mizito hali ambayo husababisha moyo kupokea kiwango kidogo cha damu.

Aidha, hypertension husababisha kupooza kwa upande mmoja wa mwili kwani damu na hewa safi hazifiki katika ubongo, vilevile ubongo hukosa damu ya kutosha hivyo kumfanya mtu kuwa masahaulifu na kuathirika katika mazungumzo kwa kimombo Dementia.

Vilevile watu wengi wenye hypertension huwa na matatizo ya figo yaliyosababishwa na shinikizo iliyoharibu mishipa inayoelekea katika figo.

Hatimaye mtu anaweza kupoteza uwezo wa kuona kutokana na kufeli kwa mishipa inayosambaza damu katika macho.

Dakta Omondi ameelezea aina mbili za Hypertension na kinga inayoweza kutumika.

Aina ya kwanza iitwayo Primary Hypertension mtu huzaliwa nayo na njia ya kuidhibiti ni kumeza dawa milele.

Aina ya pili huitwa Secondary hypertension ambayo husababishwa na mishipa ya figo ambayo hufanyiwa upasuajia ua kuongezeka au kupungua kwa homoni mwilini.

Ripoti iliyotolewa mwaka jana na Shirika la Afya Duniani WHO, inaonyesha kuwa humu nchini takriban watu elfu tatu, mia saba ishirini na wawili huaga dunia kutoka na ugonjwa huo, hivyo kuorodhesha Kenya kuwa nambari 47 duniani katika mataifa yenye idadi kubwa ya wanaoaga dunia kutokana na hypertension. 

Hatimaye Dakta Omondi anatoa wito kwa watu kuwa makini kuhusu vyakula wanavyovila, mfano kupunguza ulaji wa nyama, pombe na chumvi katika chakula. Aidha anawashauri kufanya mazoezi na kufanyiwa uchunguzi na daktari mara kwa mara kwani ugonjwa huo hauna dalili.