Oparesheni ya kuwaondoa ombaomba na watu wenye ulemavu katikati ya jiji la Nairobi kutekelezwa

Oparesheni ya kuwaondoa ombaomba na watu wenye ulemavu katikati ya jiji la Nairobi kutekelezwa

 

Oparesheni ya kuwaondoa watu wanaombaomba na wenye ulemavu katikati ya jiji la Nairobi, inatarajiwa kuendeshwa kesho. Mmoja wa wanachama wa Kamati ya Elimu, Vijana na Jinsi katika Kaunti hii, Janet Ouko amesema mpango huo utaendeshwa na serikali ya kaunti kwa ushirikiano na Baraza la Watu Wenye Ulemavu.

Amesema asilimia themanini ya watu wanao-ombaomba ni wenye ulemavu ambao wanatumiwa na wafanyabiashara fulani kuwalaghai wananchi. Kadhalika ameongeza kuwa watakaokamatwa watapelekwa katika kituo cha kurekebishia tabia eneo la Waithaka, Dagoretti.

Aidha amesema wengine ambao ni raia wa nchi jirani ya Tanzania watarejeshwa nchini mwao.