array(0) { } Radio Maisha | KAA imesitisha utekelezwaji wa mpango wa kuongeza ada ya uegeshaji magari katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta JKIA

KAA imesitisha utekelezwaji wa mpango wa kuongeza ada ya uegeshaji magari katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta JKIA

KAA imesitisha utekelezwaji wa mpango wa kuongeza ada ya uegeshaji magari katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta JKIA

Mamlaka ya Kitaifa ya Viwanja vya Ndege KAA imesitisha utekelezwaji wa mpango wa kuongeza ada ya uegeshaji magari katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta JKIA kufuatia malalamiko yaliyoibuliwa kufuatia agizo hilo. KAA imetanga hayo kupitia mtandao wake wa Twitter, na kusema inaendeleza mashauriano na washikadau katika sekta hiyo.

Mamlaka hiyo iliongeza ada za za huduma za uwekezaji katika viwanja vya ndege nchini lakini hatua hiyo haikupokelewa vyema. Shirika la Wanaharakati la Wakfu wa Nairobi liliwasilisha kesi kupinga ada hizo mpya na kusema zilikuwa ghali mno, na kwamba wananchi hawakushirikishwa kabla uamuzi huo kutolewa.

Kulingana na ada hizo mpya, wamiliki wa magari wangelipia shilingi mia moja kwa kuegesha magari kwa dakika ishirini katika uwanja wa JKIA, shilingi 250 kwa kati ya dakika ishirini na arubaini na shilingi 350 kwa takriban saa moja. Ada hizo mpya zilitarajiwa kutekelezwa kuanzia tarehe 15 Aprili.