array(0) { } Radio Maisha | LSK kimewasilisha ombi katika Mahakama Kuu kuitaka izuie shughuli ya hati-miliki na stakabadhi nyingine katika Wizara ya Ardhi kutolewa kwa njia ya kidijitali

LSK kimewasilisha ombi katika Mahakama Kuu kuitaka izuie shughuli ya hati-miliki na stakabadhi nyingine katika Wizara ya Ardhi kutolewa kwa njia ya kidijitali

LSK kimewasilisha ombi katika Mahakama Kuu kuitaka izuie shughuli ya hati-miliki na stakabadhi nyingine katika Wizara ya Ardhi kutolewa kwa njia ya kidijitali

Chama cha Wanasheria LSK kimewasilisha ombi katika Mahakama Kuu kuitaka izuie shughuli ya hati-miliki na stakabadhi nyingine katika Wizara ya Ardhi kutolewa kwa njia ya kidijitali. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa katika Mahakama ya Milimani , LSK imeitaka mahakama kutoa agizo la kuizuia wizara hiyo dhidi ya kutekeleza mfumo huo hasa uhamishaji wa ardhi.

Kadhalika inataka Waziri Farida Karoney aagizwe kubuni jopokazi litakalowajumuisha washikadau wote ambao wameathirika na mfumo huo wa usajili wa ardhi kwa njia ya kielektroniki.

Wanasema jopokazi hilo linafaa kupewa jukumu la kuandaa miongozo kuhusu utekelezaji wa mfumo huo katika muda wa miezi miwili ijayo. LSK imeeleza wasiwasi kwamba notisi iliyotolewa na Wizara ya Ardhi imechangia kusitishwa kwa utekelezaji wa shughuli katika wizara hiyo kwa njia ambayo si ya kielektroniki katika ofisi za usajili jijini Nairobi na eneo la Kati.