array(0) { } Radio Maisha | DAKTARI AZUILIWA KWA KUWAPA WANARIADHA SUMU

DAKTARI AZUILIWA KWA KUWAPA WANARIADHA SUMU

DAKTARI AZUILIWA KWA KUWAPA WANARIADHA SUMU

NA STEPHEN MUKANGAI

Shirika la kupambana na matumizi ya dawa haramu miongoni mwa wanamichezo (ADAK ) linaendelea kumzuilia mshukiwa anayedaiwa kuwauzia wanariadha dawa zilizo pigwa marufuku eneo la bonde la ufa.

DAKTARI Samuel Kosgei Cheptoo anayemiliki duka la dawa la Eldosako Chemistry mjini Eldoret, amekuwa akichunguzwa baada ya mwanariadha mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe kudai kuwa alimdunga sindano ya dawa aina ya EPO iliyosababisha atemwe nje ya kikosi cha Kenya kilicho shiriki mashindano ya Jumuia ya Madola.

MSHUKIWA huyo anadaiwa kushirikiana na walaghai ambao huwashawishi wanariadha kutumia dawa hizo kwa kuwadanganya kuwa dawa zenyewe hazionekani kwenye chembechembe za damu baada ya matumizi.

AFISA mkuu Mtendaji wa Shirika hilo la kupambana na matumizi ya dawa haramu Japhter Rugut ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.