Mvua kubwa yaendelea kunyesha semehu tofauti nchini

Mvua kubwa yaendelea kunyesha semehu tofauti nchini

Mwanamke pamoja na mtoto wa shule ya chekechea wamefariki maji baada ya kusombwa na mafuriko walipokuwa wakivuka mto Ilenye Kaunti ya Kitui.

Mkuu wa polisi eneo la Mwingi John Nyamu amesema kuwa tayari miili ya wawili hao imetolewa mtoni humo.

Taarifa hii inajiri wakati athari za mafuriko zikiendelea kushuhudiwa maeneo tofauti nchini.

Inaarifiwa kuwa miili wanafunzi wawili wa kidato cha pili kwenye shule ya Upili ya Gavernor eneo la Longonot wamepatikana katika mtaro eneo hilo baada ya kusombwa na mafuriko kwenye barabara ya Mai Mahiu - Narok usiku wa kuamkia Jumatano.