Aliyekuwa Mbunge Mathew Lempurkel akamatwa kwa madai ya kutaka kutekeleza mauaji

Aliyekuwa Mbunge Mathew Lempurkel akamatwa kwa madai ya kutaka kutekeleza mauaji

Aliyekuwa Mbunge wa Laikipia Kaskazini Mathew Lempurkel anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 14 au 15 mwezi Machi mwaka huu, baada ya kukamatwa na maafisa wa polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kaunti ya Laikipia Simon Kipkeu, Lempurkel, alikamatwa kwa madai ya kupanga kutekeleza mauaji. 

Mbunge huyo wa zamani anatuhumiwa kuwa mnamo tarehe 31 mwezi Julai mwaka 2016,  alitishia kukiteketeza Kituo cha Polisi cha Rumuruti, ili kuhakikisha mshukiwa mmoja anayezuiliwa kituoni humo anaachiliwa. 

Atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika. Lempurkel alikamatwa punde baada ya mahakama mjini Nanyuki kuamua kwamba ana kesi ya kujibu katika kesi nyingine ya uchochezi dhidi yake. Hakimu Mkuu Lucy Mutai alisema upande wa mashtaka uliwasilisha kesi nzito dhidi yake.