Shughuli ya kuwasajili makurutu wa KDF yakamilika Kakamega

Shughuli ya kuwasajili makurutu wa KDF yakamilika Kakamega

Shughuli ya kuwasajili makurutu wa kujiunga na kikosi cha jeshi, KDF Kaunti ya Kakamega imekamilika, huku ikibainika kuwa vijana wengi walikosa nafasi ya kujiunga na kikosi hicho licha ya kuwa na vyeti vinavyohitajika.

Akizungumza kwenye uwanja wa Solyo Eneo Bunge la Shinyalu, Afisa aliyeongoza shughuli hiyo, Kanali Paul Kindochimu amesema vijana wengi wamepatikana na alama za majeraha mwilini huku wengine wakikosa meno yote kinywani, jambo lililowasababisha kukosa nafasi.

Shughuli hiyo inayotarajiwa kukamilika Machi 13 kote nchini inalenga kuwasajili makurutu elfu mbili.