Salim Lone awakosoa wanaopinga kuapishwa kwa Raila

Na, Beatrice Maganga
 
Kinara wa NASA, Raila Odinga, amesisitiza kuwa mpango wa kumwapisha Jumanne wiki ijayo ungalipo, huku akipuuza kauli kwamba huenda hatua hiyo ikaibua taharuki na migawanyiko nchini. Kutika taarifa iliyotumwa na Msemaji wake, Salim Lone, Raila amesema licha ya kwamba amekuwa tayari kwa mazungumzo hakuna jitihada zilizochukuliwa na serikali yake kutuliza hali nchini, hasa tangu kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta. Amesema kuapishwa kwake hakutakiuka sheria na kusema kuwa kutazuia migawanyiko zaidi nchini. Ameongeza kuwa yu tayari kushiriki mazungumzo ambayo yanaweza kudumisha imani kuhusu Tume ya Uchaguzi, IEBC na kufanikisha uchaguzi huru siku za usoni.
Hayo yanajiri huku Muungano wa NASA ukiwaandikia barua magavana kumi na mmoja ukiwataka kubainisha eneo la kumwapishia Raila siku ya Jumanne wiki ijayo. Magavana walioandikiwa barua hizo ni Anyang' Nyong'o wa Kisumu, Hassan Joho wa Mombasa, Okoth Obado, Migori, Wyclif Oparanya Kakamega, Wilber Otichilo wa Vihiga, Amason Kingi wa Kilifi, Cyprian Awiti, Homabay, Sospeter Ojamong, Busia, Cornel Rasanga Siaya na Charity Ngilu wa Kitui.
Kaunti hizo ni zile ambazo tayari zimeidhinisha kubuniwa kwa mabunge ya wananchi. Ikumbukwe NASA imetangaza kutomtambua Rais Uhuru Kenyatta aliyeapishwa wiki iliyopita kuhudumu kwa hatamu ya pili na ya mwisho.
Licha ya hayo, mzozo unazidi kutokota kuhusu suala la kumwapisha Raila huku baadhi ya wanachama wa Wiper, ambacho ni kimojawapo cha vyama tanzu vya NASA wakidai hawajafahamishwa rasmi kuhusu mipango hiyo. Seneta wa Makueni, Mutula Kilonzo Junior hata hivyo amesema Gavana wa Makueni, Kivutha Kibwana anatarajiwa kupewa ujumbe wa mwaliko. Mutula amesema baadaye wananchi watafahamishwa iwapo kinara wa chama hicho, Kalonzo Musyoka ambaye yuko nje ya nchi atahudhuria hafla hiyo ama la. 
Tayari serikali ya Marekani imemwomba Raila kutojiapisha. Naibu Katibu Mkuu katika Idara ya Masuala ya Afrika, Donald Yamamoto ameonya kuwa mpango huo huenda ukazidisha mgawanyiko nchini. Akizungumza baada ya kufanya mkutano wa faragha na vinara wa NASA, Yamamoto ameahidi kuhakikisha mazungumzo yanaandaliwa baina ya Kenyatta na Raila ili kutatua utata wa kisiasa ulioko nchini. Aidha kwa mujibu wa waliohudhuria kikao hicho, serikali ya Marekani imewaonya wanaopinga mazungumzo kuandaliwa baina ya serikali na upinani kuwa huenda wakawekewa vikwazo vya kutozuru Marekani.